KOCHA mpya wa Manchester United Louis van Gaal "LVG" aliwasili kwenye uwanja wa mazoezi wa Manchester United, Carrington siku ya Jumatano tayari kwa kuanza kuikochi timu hiyo.
Mdachi hiyo alifanikiwa kukwepa kamera za mapaparazi kwenye lango kuu, lakini baadae picha zake zikaonekana kwenye akauti ya Twitter ya klabu hiyo akiwa sambamba na msaidizi wake Ryan Giggs pamoja na mtendaji mkuu wa United Ed Woodward.
Kocha huyo hakutaka kuwa na likizo baada ya kumaliza majukumu yake ya kombe la dunia akiwa timu ya taifa ya Holland na badala yake alitumia mapumziko ya siku nne tu kabla ya kuelekea Manchester.
Van Gaal, 62 atatambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari saa 9 mchana kwenye mkutano utakaofanyika Old Trafford kabla ya kuelekea Marekani siku ya Ijumaa kwenye ziara ya maandalizi ya msimu ujao.
United itacheza na Los Angeles Galaxy, Roma, Inter Milan na Real Madrid, wakati mechi ya kwanza ya kirafiki kwa Van Gaal katika dimba la Old Trafford itakuwa mwezi ujao tarehe 12 pale itakapomenyana na Valencia ya Hispania.
Siku nne baadae United itaanza kampeni yake ya kusaka taji la Barclays Premier League dhidi ya Swansea.
Louis van Gaal "LVG"
Ryan Giggs, Van Gaal pamoja na Ed Woodward.
Ryan Giggs na Van Gaal
Van Gaal pamoja na Ed Woodward.
Ryan Giggs, Van Gaal pamoja na Ed Woodward
Ndege ya kukodi iliyomleta Van Gaal
Van Gaal baada ya kushuka kwenye ndege
Van Gaal na Ed Woodward.
Mchezaji mpya wa Herrera akiwasili mazoezini