Thursday, July 10, 2014

Mwalimu Dodoma matatani kwa tuhuma za kuua mwalimu mwenzake kisa deni la buku moja



Mwalimu Dodoma matatani kwa tuhuma za kuua mwalimu mwenzake kisa deni la buku moja
JESHI la Polisi Mkoani Dodoma linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Hombolo Justus Jackson (28) kwa tuhuma ya kumuua mwalimu mwenzie kwa kukataa kulipa sh. 1,000 ya bili ya umeme aliyotakiwa kuchangia marehemu. 
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, David Missime amemtaja mwalimu aliyeuwawa kuwa ni Freddy Ndahani (29) mwalimu wa shule ya Hombolo.
Kamanda  Misime amesema walimu hao wote wawili wanalikuwa wakiishi katika nyumba moja na walikuwa wakichangia bili ya umeme katika nyumba hiyo. 
 Amesema katika mabishano walimu hao waliingia katika ugomvi na inadaiwa Mwalimu  Freddy alisukumwa katika ukuta na kupoteza maisha papo hapo. 
 Kwa mujibu wa Kamanda Misime Mtuhumiwa huyo ameshakamatwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika kwa upelelezi.