Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Jordan Rugimbana leo amezindua rasmi utoaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi Wilaya ya Kinondoni, na kuwa mtu wa kwanza kupokea kitambulisho chake mbali na kuwakabidhi wananchi 22 Vitambulisho vyao kutoka Kata ya Saranga mtaa wa Matangini.
Mkuu wa Wilala ya Kinondoni akiwasili leo katika Kata ya Saranga Mbezi tayari kuzindua zoezi la utoaji Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Kata ya Saranga, Mbezi Dar-es-salaam
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana akikabidhiwa Kitambulisho chake na Afisa Usajili Wilaya ya Kinondoni Ndugu Abdulrahman Muya baada ya kukamilisha hatua za mwisho za uhakiki leo Kata ya Saranga Mbezi Dar-es-salaam. Kushoto ni Bw. Dickson Mbanga Weiss Afisa Usajili Kinondoni
Mmoja wa wananchi wa Kata ya Saranga akiongozwa na Afisa Usajili wa NIDA kukamilisha hatua za mwisho za kuhakiki taarifa zake kabla ya kukabidhiwa kitambulisho chake leo, Kata ya Saranga Mbezi
Hapa anamkabidhi mmoja wa wananchi Bi. Chiku Issa Waziri kitambulisho cha Taifa, akishuhudiwa na Maafisa Usajili katika Wilaya Bw. Dickson Mbanga Weiss na Bw. Abdulrahman Muya