Wednesday, July 02, 2014

MKURUGENZI MKUU WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF WILLIAM ERIO AKAGUA BANDA LA PPF KUJIONEA UTENDAJI KAZI KATIKA MAONYESHO YA SABASABA




MKURUGENZI MKUU WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF WILLIAM ERIO AKAGUA BANDA LA PPF KUJIONEA UTENDAJI KAZI KATIKA MAONYESHO YA SABASABA
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mhe William Erio akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa Mfuko huo wakati alipotembelea Banda laa PPF kujionea utendaji kazi wa Wafanyakazi wake katika maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam yanayoendelea Kufanyika katika Viwanja vya Mwl Nyerere.
Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa Pensheni wa PPF, Mhe William Erio akiteta jambo na wafanyakazi wa PPF wakati alipotembelea Banda la PPF kujionea utendaji kazi wa Wafanyakazi wake. Kulia ni Meneja Uhusiano na Masoko wa PPF, Bi Lulu Mengele na Katikati ni Mbaruku.

Mmoja wa Wateja Wa Mfuko wa Pensheni wa PPF akifurahia huduma aliyopewa na Afisa Huduma Kwa Wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Jackline Jackson wakati mteja huyo alipotembelea Banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Kibiashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba.

Afisa Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anna Shayo akimuhudumia mteja aliyefika katika Banda la PPF kwaajili ya kupata maelekezo juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko huo wa PPF.
Afisa Mafao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Hellen Mollel (kushoto) akirufahia jambo na mmoja wa wateja wa PPF aliyefika katika banda la PPF kwenye Maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja hivyo vilivyopo Barabara ya Kilwa Jijini Dar Es Salaam.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakimsikiliza kwa makini mmoja wa mteja aliyefika katika banda la PPF kwaajili ya kujiunga na Mfuko huo wa Pensheni wa PPF katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea kufanyika.
Afisa Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa PPF, Mohamed Siaga akitoa maelekezo kwa mteja aliyefika kwenye dawati lake kwaajili ya kupata maelekezo juu ya huduma mbalimbali za mfuko wa PPF katika maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam.Picha zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog