Thursday, July 10, 2014

MGOMBEA URAIS WA MSUMBIJI ATUA TANZANIA KUSAKA KURA, AKUTANA NA MAMA MARIA NYERERE KUOMBA BARAKA



MGOMBEA URAIS WA MSUMBIJI ATUA TANZANIA KUSAKA KURA, AKUTANA NA MAMA MARIA NYERERE KUOMBA BARAKA
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimlaki mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha Ukombozi cha FRELIMO, Mhe Filipe Nyusi alipowasili leo jioni Julai 9, 2014, kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya ziara ya siku tatu, kusaka kura kwa wananchi wa Msumbiji wanaoishi Tanzania, kufuatia kampeni za Urais zinazoendelea nchini kwake.
Mgombea huyo wa Urais Filipe Nyusi akimsalimia Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia alifika Uwanja wa Ndege pamoja na Kinana. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.
 Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Frelimo Filipe Nyusi akisalimiana na wana-CCM waliofika kumlaki Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. Kulia ni Mwenyeji wake, Abdulrahman Kinana
 Nyusi akidhihirisha furaha kwa mapokezi aliyopata

 Mgombea huyo wa Urais wa Msumbiji akiwa na Mwenyeji wake, Kinana wakati wa mapokezi yaliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere
Filipe Nyusi akizungumza na waandishi wa habari baada ya mapokezi, Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. 

 Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mama Maria Nyerere (watatulkushoto) akiwa na ugeni wa mgombea huyo wa Urais nchini Msumbiji, Filipe Nyus (wapili kushoto), nyumbani Mwalimu, Msasani, Dar es Salaam. Kushoto ni Kinana 
 Mama Maria Nyerere akimsalimia Mtoto wa Rais wa Kwanza wa Msumbiji Samora Machel, Samora Samora ambaye alifuatana na mgombea huyo wa Urais wa Msumbiji.
 Mama Maria Nyerere akizungumza na mgombea huyo wa Urais wa Msumbiji Filipe Nyus (wapili kushoto) na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana
 Nyusi na Kinana wakimsikiliza kwa makini Mama Maria Nyerere wakati wa mazungumzo hayo
Samora Samora akizungumza na Binti wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, wakati wa ugeni huo nyumbani kwa  Mama Maria Nyerere, Msasani Dar es Salaam. Picha zote na Bashir Nkoromo