Wednesday, July 09, 2014

Mfalme wa reggae Ras Jhikoman kutoka Bagamoyo,Tanzania atua mjini Tubingen,Ujerumani



Mfalme wa reggae Ras Jhikoman kutoka Bagamoyo,Tanzania atua mjini Tubingen,Ujerumani
 Mwanamuziki nyota wa reggae barani Afrika Jhiko Manyika aka Jhikoman kutoka Bagamoyo,Tanzania amewasili mjini Tubingen,Ujerumani kwa ajili ya kushiriki katika maonyesho makubwa ya 5th International African Festival Tübingen 2014, yatakayoanza 17 julai 2014 mpaka 20 Julai 2014 katika viwanja ya Festplatz, mjini Tübingen. 
Watayarishaji wa maonyesho hayo Afrikaktiv.org wamemtaja mwanamuziki Jhikoman kuwa ni nyota inayong'aa kutoka Afrika na wamemwalika kwa ajii ya kuja kuzidisha mwangaza katika soko la ulaya. 
Mkurugenzi wa maonyesho hayo Madam Susan Tatah alisema kuwa ujio wa mwanamuziki Jhikoman nchini Ujerumani unazidisha uhusiano mzuri katika sekta ya sanaa na utamaduni kati ya Ujerumani na Tanzania pia Afrika kwa ujumla.
Madam Susan Tatah alisema ujio wa Jhikoman una maana kubwa kwa wajerumani kwa mwanamuziki huyo anatoka katika mji wa Bagamoyo ambako ndipo palikuwa makao makuu ya serikali ya ukoloni ya kijerumani na ndipo Wajerumani walipojenga shule ya mwanzo Afrika Mashariki, Madam Susan Tatah alisema Jhikoman pia atatia sahini
mkataba wa ushirikiano wa kudumu wa "Cultural Exchange program" pamoja Afrikaktive pia na mji wa Tübingen.