Mwanamuziki maarufu ambaye pia ni mbunge nchini Somalia, Saado Ali Warsame amepigwa risasi na kufa na wanamgambo. Aliuawa pamoja na mlinzi wake, katika shambulio la kutumia gari mjini Mogadishu. Msemaji wa kundi la al-Shabaab, ameshambuliwa kutokana na sababu za kisiasa na sio muziki wake.
Mwandishi wa BBC mjini Mogadishu Mohammed Moalimu amesema huyu ni mbunge wa nne kuuawa mwaka huu. Bi Warsame alipata umaarufu enzi za utawala wa rais wa zamani Siad Barre, aliyeondolewa madarakani mwaka 1991. Aliishi uhamishoni nchini Marekani kwa muda mrefu na alirejea mwaka 2012 na kuwakilisha ukoo wake katika bunge jipya la Somalia. Mwandishi wa BBC Idhaa ya Kisomali Abdullahi Abdi anasema Bi Warsame atakumbukwa zaidi kwa muziki wake. Alikuwa mmoja wa wasomali wanawake wachache aliyepanda jukwaani bila kujifunika kichwa na mara nyingine kuvaa suruali, jambo ambalo sio la kawaida kwa wanawake wa Somalia, amesema Abd