HOLLAND imefanikiwa kunyakua kitita cha dola milioni 22 baada ya kuinyuka Brazil na kuibuka mshindi wa tatu wa Kombe la dunia 2014.
Brazil iliyoshika nafasi ya nne nayo haitatoka mikono mitupu, inaambulia dola milioni 20.
Kikosi cha Holland baada ya kuwa mshindi wa tatu
Holland walifanikiwa kuwabana wenyeji na kupata ushindi wa mabao 3-0 mawili yakitinga katika kipindi cha kwanza na moja kipindi cha pili.
Hii inakuwa zawadi nzuri kwa kocha Loius van Gaal ambaye ameagana rasmi na kikosi hicho akielekea kwenye kibarua chake kipya cha kuikochi Manchester United.
Katika kuelekea mechi hii, Van Gaal aliwaomba wachezaji wake wampe zawadi nzuri ya kumaliza michuano hii bila kufungwa hata mchezo mmoja katika muda wa kawaida (ukiondoa hatua ya bahati nasibu ya mikwaju ya penalti).
Bao la kwanza la Holland lilifungwa na Robin van Persie kwa njia ya penalti kunako dakika ya tatu baada ya Thiago Silva kumwangusha Robben kwenye kisanduku cha hatari.
Van Persie akifungua kitabu cha magoli
Kipa Julio Cesar anaruka bila mafanikio kuzuia penalti
Van Persie akishangilia Dirk Kuyt
Beki wa kati wa Holland Daley Blind aliifungia timu yake bao la pili katika dakika ya 17 kufuatia makosa ya David Luiz.
Daley Blind anapachika wavuni bao la pili
Wakati mpira ukionekana utamalizika kwa bao 2-0, Georginio Wijnaldum akaifungia Holland bao la tatu.
Georginio Wijnaldum akifunga bao la tatu
Holland wanashangilia bao la tatu
Julio Cesar baada ya bao la tatu
Benchi la akiba la Brazil ...huzuni tupu
Brazil: Cesar, Maicon, Silva, Luiz, Maxwell, Gustavo (Fernandinho 46), Paulinho (Hernanes 56), Ramires (Hulk 72), Oscar, Willian, Jo.
Holland: Cillessen (Vorm 90+3), Kuyt, De Vrij, Vlaar, Martins Indi, Blind (Janmaat 70), Clasie (Veltman 89), Wijnaldum, de Guzman , Robben, Van Persie