"Nikiwa njiani na hata baada ya kutuas JFK, nilikuwa nawasiliana na wifi. Alionekana kama mtu aliyekata tamaa na alikuwa akiniuliza niko wapi kila wakati, nilikuwa nikisubiri ndege hapo kwa saa kama mbili. Bahati mbaya ni kwamba baada ya kucheck inn (kuidhinishwa kusafiri na kuingia sehemu ya kusubiria ndege), gurudumu lake moja lilipasuka," alisema.
"Hili jambo halikuwa la kawaida kwasababu ilibidi sasa tushuke na tusubiri tena kwa saa kama mbili ili tubadilishiwe ndege, na wakati nikiwa bado uwanjani hapo JFK, ilikuwa kama saa 8:00 mchana, nilipata simu kutoka kwa wifi akiniambia 'Mage we have lost Daudi' (Margaret, tumempoteza Daudi (Ballali)."
Alisema hakuwa na cha kufanya zaidi ya kuendelea na taratibu za safari na kwamba alipowasili Washington muda wa jioni alikwenda moja kwa moja kwenye nyumba ya kuhifadhia maiti ya Vo Funeral Home ambako aliwakuta wanafamilia, akiwamo Mama Muganda, watoto wa Marehemu Rahel na Octavio pamoja na wauguzi wawili na madaktari wakiwa wamezunguka kitanda cha marehemu, kabla ya mwili wake kuhifadhiwa.
Alisema baada ya hapo walirejea nyumbani na kuanza kupanga taratibu za mazishi, ambayo yalifanyika Mei 23, 2008 katika makaburi ya Gate of Heaven eneo la Silver Spring, Maryland, Marekani, huku mumewe, Dk Mpango akiwa miongoni mwa walioongoza ibada ya maziko ya kiongozi huyo.
Umahututi wake
Baadhi ya ndugu wa Ballali wanasema kubadilika ghafla na kuwa mahututi kuliwashtua kutokana na kutokuwapo kwa taarifa za mapema kuhusu ugonjwa wake.
Wanasema Ballali aliondoka Agosti 2007 kwenda Marekani akiwa mzima na hawakuwa na taarifa zozote kwamba ni mgonjwa, lakini walishtushwa na taarifa za kuugua kwake ghafla kiasi cha kuambiwa kwamba alikuwa mahututi.
Wanasema Ballali aliondoka Agosti 2007 kwenda Marekani akiwa mzima na hawakuwa na taarifa zozote kwamba ni mgonjwa, lakini walishtushwa na taarifa za kuugua kwake ghafla kiasi cha kuambiwa kwamba alikuwa mahututi.
Ballali alilazwa katika Hospitali ya Massachusetts, Boston mwishoni mwa Agosti 2007, wakati alipokwenda kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake na tangu wakati huo afya yake haikuimarika hadi alipofariki dunia, Mei 16, 2008 akiwa nyumbani kwake Washington DC.Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea......