Katibu wa Bunge Dr Thomas Kashililah ambae pia ni Katibu Mkuu wa CPA Barani Afrika akisikiliza maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa CPA duniani,Dr William Shija wakati alipotembelea Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo London.Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa chama hicho Bw.Joe Omorodin na kulia ni Mkuu wa Itifaki katika ofisi ya Bunge,Bw.Demetrius Mgalami.
Katibu wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola tawi la Uingereza,Bw.Andrew Tuggey akitoa ufafanuzi wa namna tawi hilo linavyojiendesha wakati Dr Kashililah (pichani kulia) na ujumbe wake walipotembelea Bunge la Uingereza kwa ziara maalum ya kikazi.wengine pichani ni watendaji mbalimbali wa CPA na Ofisi ya Bunge.
Dr Kashililah akitoa zawadi kwa mwenyeji wake katika Bunge la Uingereza,Bw.Andrew Tuggey wakati alipotembelea Bunge hilo jana.