Meneja Masoko wa kampuni ya Megatrade Ivestment Goodluck Kway kulia, akimkabidhi msaada wa vyakula diwani wa kata ya sokoni one Michael Kivuyo kwaajili ya shule za msingi katika kata hiyo ambazo ni shule ambazo zinaukosefu mkubwa wa chakula cha wanafunzi hali inayopeleka masomo kudorora na wanafunzi kuzimia ovyo kwa ajilii ya njaa mashuleni hali hiyo ilipelekea kampuni hiyo kujitolea msaada uliogharimu kiasi cha shilingi Milioni moja,msaada huo ni Magunia ya mahindi,maharagwe na mafuta ya kula, jana jijini Arusha
Meneja Masoko wa kampuni ya Megatrade Ivestment Goodluck Kway kulia akimkabidhi gunia la maharagwe diwani wa kata ya sokoni one Michael Kivuyo jana jijini Arusha kwaajili ya shule za msingi katika kata hiyo,shule zilizonufaika na msaada huo ni shule ya Sokoni 1,Sinoni,Ukombozi,Engosengiu na Sinoni
Diwani wa kata ya sokoni one Michael Kivuyo akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ukombozi Bi.Fatuma Mashombo gunia la mahindi kwaajili ya wanafunzi wa shule yake. (Pamela Mollel jamiiblog).