Thursday, July 10, 2014

DKT.MAGUFULI AENDELEA NA ZIARA MWANZA NA SINGIDA AZINDUA KIVUKO CHA MV.TEMESA NA KUKAGUA DARAJA LA MBUTU


DKT.MAGUFULI AENDELEA NA ZIARA MWANZA NA SINGIDA AZINDUA KIVUKO CHA MV.TEMESA NA KUKAGUA DARAJA LA MBUTU
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea na ziara ya kikazi Jijini Mwanza ambapo leo amezindua kivuko cha MV.TEMESA kitakachofanya safari zake kutokea Luchele kupitia mwambao wa ziwa Victoria. 
Kivuko hiki kimetengenezwa/kimejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 640 na ni kivuko pekee chenye mwedo kasi kuliko vyote Tanzania, kina uwezo wa kubeba tani 65. 
Wengine walioshiriki katika uzinduzi huo ni Mhandisi Mussa Iyombe (Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi), Mhandisi Evarist Ndikilo (Mkuu wa Mkoa wa Mwanza), Mkuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Bodi zilizo chinin ya Wizara ya Ujenzi, Wakurugenzi wa Wizara ya Ujenzi, Wafanyakazi wa TEMESA, wafanyakazi wa SUMATRA pamoja na wananchi. Aidha, Dkt.Magufuli amesafiri mpaka Singida na kuelekea kwenye ujenzi daraja la Mbutu linalojengwa na Wakandarasi Wazalendo - Mbutu JV kwa gharama ya shilingi bilioni 12. 
Kwa ujumla kazi za ujenzi wa daraja zimefikia asilimia 95 ambapo deki la daraja limekamilika. Ukubwa wa daraja hilo umechukua takribani urefu wa kilomita tatu. Katika ukaguzi huo, Waziri wa Ujenzi aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Wilaya, Katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Wenyeviti wa Bodi na Wananachi.
Dkt.Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kivuko,wengine ni Mhandisi Everist Ndikilo (Mkuu wa Mkoa wa Mwanz, Mkuu wa Wilaya, Mhandisi Mussa Iyombe (Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi), Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Wakurugenzi wa Wizara ya Ujenzi, Wenyeviti wa Bodi mbalimbali na wananchi.
Dkt.Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mkuu wa Wilaya wakitoka ndani ya kivuko.
Dk.Magufuli, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Wilaya wakipozi ndani ya kivuko cha Mv.TEMESA kwa pamoja na wafanyakazi wa SUMATRA na TEMESA.
Dkt.Magufuli akifanya ukaguzi daraja la Mbutu