Wednesday, July 23, 2014

JK afungua nyumba za Watumishi wa Afya Matemanga, Tunduru, zilizojengwa na Mkapa Foundation



JK afungua nyumba za Watumishi wa Afya Matemanga, Tunduru, zilizojengwa na Mkapa Foundation
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kiwete akiteta jambo na mkazi wa kijiji cha Ligela wilayani Namtumbo Bwana Edwin Ngonyani wakati alipokuwa anahitimisha ziara yake wilayani humo.Bwana Ngonyani ambaye alipata ulemavu baada ya kupoteza miguu yote miwili katika ajali ya moto alimweleza Rais kuwa anapata taabu ya kutafuta riziki kwakuwa anatambaa kwa taabu.Rais Kikwete alitoa ahadi ya kumsaidia mlemavu huyo ili aweze kujikimu kimaisha.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi wa kijiji cha Matemanga wakati wa hafla ya uzinduzi nyumba 480 za watumishi wa umma zilizojengwa na Taaasisi ya Benjamin W.Mkapa kwa ushirikiano na Wizara ya Afya
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin w.Mkapa Dkt  Ellen Mkondya Senkoro(kushoto) akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete michoro na ramani za nyumba za watumishi wa afya zilizojengwa na taasisi hiyo wkati hafla ya uzinduzi wa nyumba hizo uliofanyika katika kijiji cha Matemanga wilayani Tunduru leo.Watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na wane kushoto ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua mradi wa nyumba za watumishi wa afya zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation katika hafla iiyofanyika katika kijiji cha Matemanga wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma leo.
Jumla ya nyumba 480 zinajengwa katika halmashauri 48 nchini na miongoni mwa nyumba hizo 40 zipo katika mkoa wa Ruvuma.Taasisi ya Benjamin Mkapa iliingia mkataba na Wizara ya Afya kutekeleza mradi wa miaka mitano(2011-2016) wa uimarishaji wa mifumo ya Huduma za afya chini ya ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kupambana na ukimwi,kifua kikuu na Malaria(Global Fund).
Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin W.Mkapa Dkt.Ellen Senkoro, Mbunge wa Jimbo la Tunduru Mhandisi Ramo Makani, Meneja wa Portfolio, Mfuko wa Dunia wa Kupambana na ukimwi,kifua kikuu na Malaria Bi. Tatajana Peterson, Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof.Anna Tibaijuka, Naibu Waziri wa TAMISEMI Aggrey Mwanri, Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Kebwe Stephen  Kebwe, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Saidi Mwambungu. Picha na Freddy Maro