Thursday, July 03, 2014

JESHI LA MAGEREZA LAIBUKA MSHINDI WA KWANZA KATIKA UTENGENEZAJI BORA WA SAMANI ZA NDANI MAONESHO YA 38 YA BIASHARA YA KIMATAIFA, JIJINI DAR ES SALAAM



JESHI LA MAGEREZA LAIBUKA MSHINDI WA KWANZA KATIKA UTENGENEZAJI BORA WA SAMANI ZA NDANI MAONESHO YA 38 YA BIASHARA YA KIMATAIFA, JIJINI DAR ES SALAAM
 Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi  Seif Idd akikabidhi zawadi ya Mshindi wa kwanza kwa Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga. Jeshi la Magereza limeibuka Mshindi wa kwanza kwa utengenezaji wa bidhaa bora za Samani za ndani katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja wa Mw. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wanaoshiriki katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa wakifurahia ushindi wa kwanza katika utengenezaji wa Samani Bora za ndani(katikati mstari wa mbele) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga akiwa ameongozana na  Washiriki wa Maonesho ya Kibiashara katika Banda la Jeshi la Magereza.
 Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza Wanaoshiriki ushindi wa kwanza kwa upande wa Samani za Ndani baada ya kutanganzwa rasmi leo katika hafla fupi ya ufunguzi wa Maonesho ya 38 ya Kibiashara ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
Cheti cha ushindi wa kwanza ambacho Jeshi la Magereza limeibuka katika utengenezaji wa Bidhaa za Samani za ndani katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea hapa Jijini Dar es Salaam. Jeshi la Magereza linasifika kwa utengenezaji wa bidhaa bora za Samani za Ndani na Ofisi hapa Nchini Tanzania. Picha zote na Lucas Mboje wa Magereza