Vijana waliopata kipaimara jana. |
Ibada hiyo iliongozwa na mchungaji Moses Shonga akisaidiana na mchungaji Tumaini Kallaghe, ambapo pia katika ibada hiyo watu waliozaliwa mwezi julai waliandaliwa keki maalumu pamoja na kufanyiwa maombi ya baraka juu ya maisha yao maombi ambayo yaliongozwa na mtume Matthew Jutta ambaye kwakushirikiana na waimbaji wengine kutoka katika huduma yake ya Worldchangers ministries. Mara baada ya ibada waumini walipata muda wa kula pamoja chakula kama ilivyoada ya kanisani hapo kila ibada iishapo.
Kanisa hilo hufanya ibada mbili ndani ya mwezi, ibada ya kwanza hufanyika kila jumapili ya kwanza ya mwezi na ibada ya pili hufanyika kila jumapili ya tatu ya mwezi, ambapo ibada zote huanza majira ya saa nane mchana.
Mtume Jutta na timu yake wakiongoza waumini kumsifu Mungu. |
Sifu Bwana pamoja na Yawe habadiliki kamwe ziliimbwa. |
Vijana wa kipaimara wakiwa ibadani. |
Mchungaji Tumaini pamoja na mchungaji Shonga wakiendesha ibada ya ubatizo. |
Ubatizo ukaanza. |
Ubatizo ukiendelea. |
Nakubatiza kwa jina la Baba na Mwana na la Roho mtakatifu Amen. |
Baada ya ubatizo baraka zikatolewa na mishumaa kuashiria kuwa nuru ya ulimwengu kwa wabatizwaji hao. |
Ikafuata tukio la kipaimara. |
Ikawa kukiri imani ya mitume na kumkataa shetani. |
Baraka za kipaimara zikatolewa. |
Mchungaji Shonga akiendelea na huduma hiyo. |
Wakiwa wenye furaha mara baada ya kupokea kipaimara. |
Wakiwa wenye furaha. |
Nyuso za furaha kwa tukio lao kufanikiwa. |
Waumini wakifurahi pamoja nao. |
Ilikuwa furaha kwakila mtu aliyefika kanisani hapo. |
Lusajo (anayepiga gitaa) akiwaongoza wenzie kuimba wimbo 'Your presence is enough to me' wa kwake Israel Houghton. |
Waliozaliwa mwezi Julai wakiwa mbele kupata baraka, pembeni ikiwa keki yao tayari kwaajili yao. |
Mwishoni vijana wa kipaimara wakaeleza machache kupitia risala yao. |
Baadhi ya vyakula vilivyokuwepo. |
Mmmh nimeshavimisi tayari kha, adimu hivi ulaya huku. |