Tuesday, July 22, 2014

CHIKAWE AWAPA SOMO VIONGOZI WA CCM NACHINGWEA

PIX 1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akizungumza na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Namikango, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi leo. Waziri Chikawe aliwataka viongozi hao kuwa na umoja ili kukipa nguvu chama chao hasa katika kipindi hiki wanapoelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambapo kila mwanachama wa chama hicho alisisitizwa kuchukua fomu wakati muda utakapofika wa kuchukua fomu hizo. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu ambapo wananchi watachagua Viongozi wa Mamlaka za Wilaya, Mamlaka za Miji midogo, Mamlaka za Miji na Halmashauri za Vijiji na Vitongoji. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nachingwea, Albert Mnali. Picha na Felix Mwagara wa WMNN.

PIX 2