Mzee wa kanisa la Waadventista wasabato mtaa wa kijenge Agrey Tumaini akigawa mahindi kwa wananchi wa kitongoji cha kitongoji cha Nyamagana kilichopo katika kijiji cha Themi ya simba wilayani Arumeru MKoani Arusha (picha na woinde shizza,Arusha
========= ====== ======
Na Woinde shizza,Arusha
Zaidi ya wananchi 50 wa kitongoji cha Nyamagana kilichopo katika kijiji cha Themi ya simba wilayani Arumeru MKoani Arusha ambao waliathiriwa na mafuriko yaliotokea mwisho mwa mwezi wa nne mwaka huu wamepatiwa msaada wa chakula na nguo kijijini hapa.
Akikabidhi chakula hicho mzee wa kanisa la Waadventista wasabato mtaa wa kijenge Agrey Tumaini alisema kuwa wameamua kuwasaidia wananchi hawa kutokana na janga ambalo liliwakuta la kuingiliwa na mafuriko ya maji ambapo yaliwasababishia nyumba pamoja na mazao yao kuezuliwa na maji hayo
Alisema kuwa wao kama kikundi cha WAMO kutoka katika kanisa hilo waliguswa sana na tatizo hili ambalo liliwatokea hivyo wakaamua kujichanga na kununua vyakula ivyo na nguo kwa ajili ya wahanga hao wa mafuriko.
Alisema kuwa wameweza kutoa gunia kumi za mahindi ,maharage kunia tatu,unga wa ugali pamoja na nguo kwa ajili ya watoto wa wananchi ambao walikubwa na janga hilila mafuriko.
"sisi tumeguswa sana na tukio hili wenzetu kukubwa na mafuriko kwa kweli wameadhirika vikubwa kwani wengine awana sehemu zakukaa wengine walikuwa wamelima mazao yao kama mahindi yaliezuliwa na mafuriko hayo yaani kiukweli hadi sasa kuna watu awajui wataishije kwa mwaka huu lakini tumeona sio vibaya iwapo tukiwasaidia ichi kidogo tulichonacho maana ata neno la mungu linasema katika mathayo uwa mlikuja na njaa nikawapa chakula,mlikuja uchi nikawavisha sasa na sisi tumeamua kuwapa ichi kidogona tunawaomba watu wengine waendelee kujitokeza kwa wingi kuwasaidia wananchi hawa kwani wapo katika mazingira magumu sana"alisema Tumaini.
Akipokwa msaada huo mmoja wa wananchi hao alietambulika kwa jina la Gidion Maganga alisema kuwa anashukuru sana kanisa hili la wa sabato kwa kuja kuwasaidia kwani kuna baadhi yao walikuwa hawajui hatima ya maisha yao kwani ata chakula kwao kupata ni tabu .
Alisema kuwa pamoja kuwa kuna baadhi yaviongozi na taasisi ambazo zimewapelekea chakula kama maindi ,magodoro pamoja na nguo lakini bado wanaitaji maada kwani mvua zile ziliwachukulia vitu vyao vingi ikiwemo mazao maindi waliokuwa wameyaifadhi ndani vyombo ,magodoro na sio ivyo tu lakini pia zileweza kumuua mwananchi mmoja.
Akizungumzia tukio hilo mwananchi mungine ambaye aliyejitaja kwa jina la Zainabu Minja alisema kuwa siku hiyo ya tukio lilitokea majira ya saa saba usiku wakati wamelala huku mvua ikinyesha ndipo gafla waliona maji mengi yamekuja na kujaa ndani ya nyumba kitu ambacho kiliwaogopesha zaidi ni pa le maji yale yalivyoanza kusomba vitu.
"yaani ndugu muandishi usione apa yaani maji yalikuja na kasi unaona hii chuma ina uzitowa kilomia ndio niliichukuwa nikaishika na uyu ni mama yangu na unamuona alivyo mzee nilimwambia ashikilie iyo chuma akashika mwishowe mikono ikafa ganzi ndipo nikachukua kanga na kumfunga kiunoni nikaunganisha na chuma ili asipelekwe na maji ila nashukuru mungu alituona pamoja vitu vilizolewa lakini sisi ni wazima kwakweli"alisema bi Zainabu
Alitoa wito kwa wananchi serekali pamoja na taasisi mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuwasiaidia kwani wapo katika halingumu sana katika kipindi hichi.