Kamisha wa Elimu nchini Prof, Eustella Bhalalusesa akikata utepe kuashiria uzinduliwa rasmi Maktaba inayo tembea Wilayani Bagamoyo.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi Teknolojia na Mawasiliano Bw John Mngodo akiwa washa Piki piki ya Miguu mitatu aina ya TOYO iliyo beba makta kama kiashirio cha Maktaba hiyo inayo tembea ipo tayari kuanza kazi.
Mkurugenzi Mkazi wa ITIDO Bi Mwawi Mlekano akimkabidi Kamisha wa Elimu nchini Prof, Eustella Bhalalusesa alioko kushoto Kadi ya TOYO iliyo undwa mahususi kuwa Maktaba inayo Tembea.
Baadhi ya wanafunzi na Walimu wa Shule za Wilayani Bagamoyo walio udhuria uzinduzi wa mpango wa ICT 4 GIRLS.
Na Madau Sixmund J. Begashe.
Kamisha wa Elimu nchini Prof, Eustella Bhalalusesa ameihasa jamii kuacha kuwakandamiza watoto wakike na kuwaona kuwa hawawezi katika kujiendeleza bali wapewe nafasi sawa kama wanavyo pewa watoto wakiume, Prof Bhalalusesa aliyasema hayo alipo kuwa akizindua mpango maalum wa kuwawezesha wanafunzi wa Wilayani Bagamoyo hasa wasichana kwa njia ya TEHAMA.
Prof Bhalalusesa ameto wito kwa wasichana hasa waliopo mashuleni kutumua vyema miradi inayo anzishwa kwa ajili yao ili kuaondoa dhanapotofu iliyojengeka dhidi yao, hata ivyo aliwahasa kuitumia vyema teknolojia hii ya mawasiliano ili kuwaletea tija na si vinginevyo.
Nae kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi Teknolojia na Mawasiliano Bw John Mngodo akizungumza na wakazi hao wa Bagamoyo alisema kuwa mchango huu wa ITIDO umekuja wakati muafaka kwani maendeleo ya TEHAMA ni ya kasi sana, hivyo amewashauri wanatanzania kuendana na kasi hii kwa maendeleo ya nchi yetu.
Akizungumza na mwandishi wa Habari hizi Mkurugenzi Mkazi wa ITIDO Bi Mwawi Mlekano alisema kuwa Taasisi yake imeona itoe mchango wake kwenye Maktaba ya Wilaya ya Bagamoyo kwa kuikarabati na Kuipatia vifaa vya ICT ili kutoa fursa kwa wanafunzi hasa wakike kutumia vifaa hivyo katika kujisomea kwani wamekuwa wakikosa fursa hiyo kwa muda mrefu.
Bi Mlekano aliongeza kuwa kwakuwa shule nyingi za Bagamoyo azina Maktaba hivyo Taasisi yake imeona ni vyema ikabuni Mabkata inayotembea na kulikabidhi Shirika la Maktaba ya Taifa ili Maktaba hiyo iweze kutoa huduma kwenye shule zilizo mbali na Maktaba ya Wilayani hapo.
Licha ya kuishukuru ITIDO kwa Mchango wa kielimu, Bagamoyo, Mwl Adbeel Kitungwa wa Shule ya Sekondari ya Bagamoyo aliishauri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini, kuanzasha mtaala wa mafunzo ya TEHAMA kwa matendo na kufanyiwa mtihani wa kitaifa kuliko hilivyo hivi sasa ambapo hakuna kipaombele katika kuwawezesha wanafuzi kimatendo.
Mpango huu wa kuwawezesha wanafunzi wa shule za Bagamoyo hususani wasichana kutumia TEHAMA katika kujiendeleza kielimu umegharimu Dola 80,000 za kimarekani zilizo fadhiliwa na Shirika la Kiswidish linalo ratibiwa na Chuo kikuu cha Stockholm cha Sweden (SPIDER) na mradi huo kutekelezwa na ITIDO, EIFL, TLSB na SLADS, Milioni 5 zilizo tolewa na ITIDO Kununulia Maktaba inayo tembea.