Monday, June 30, 2014

WAKAZI WA JIJI LA DAR WAOMBA VODACOM EXPO IFANYIKE MARA MBILI KWA MWAKA.



WAKAZI WA JIJI LA DAR WAOMBA VODACOM EXPO IFANYIKE MARA MBILI KWA MWAKA.
Wakazi wa jiji la Dar es salaam na wateja wa Vodacom na watanzania kwa ujumla wamepata fursa ya kununua bidhaa mbalimbali kupitia gulio la"Vodacom Expo" lililofanyika kwa siku mbili mfululizo katika viwanja vya Leaders Club.
 Sekta ya mawasiliano nchini inakua kwa kasi kila kukicha na kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi tofauti na zamani. Kampuni ya Vodacom kwa kulitambua hilo inafanya jitihada za kuhakikisha wateja wake wote wananufaika na teknologia ya kisasa ya huduma za mawasiliano kwa urahisi ili kuendana na kasi hiyo. 
 Kama ilivyotarajiwa umati mkubwa ulijitokeza viwanjani hapo kujipatia bidhaa za kisasa za mawasiliano na zenye ubora kwa bei nafuu zaidi kuliko zile za dukani. 
Wateja na wananchi kwa ujumla walifurika katika viwanja hivyo kwa ajili ya manunuzi wa bidhaa mbalimbali za mawasiliano. Kwa mujibu wa mkazi wa kijitonyama jijini Dar es Salaam Juma Khamis alisema alifurahishwa na kazi nzuri wanayoifanya kampuni hiyo kwa kuwajali wateja wake na kutambua ni kitu gani wanahitaji. 
Kulingana na changamoto za hali ya kiuchumi zinazowakabili miongoni mwa wateja wengi si kila mtu anaweza kumudu gharama ya baadhi kama zitauzwa kwa bei zinazouzwa dukani. 
 Aliendelea kusema kuwa "Tukio hili limekuja wakati muafaka kwani nilikuwa na mipango ya kununua simu mpya, nawashukuru Vodacom kwani nimeweza kununua simu na fedha nyingine zimebaki. Bidhaa za hapa ni bora na ni za kisasa sina mashaka nazo, ningependa zoezi hili liwe linafanyika angalau mara mbili au tatu hivi kwa mwaka badala ya mara moja kama ilivyo sasa." 
 Kivutio kikibwa katika tukio hili ni unafuu wa bei za bidhaa huku zikiwa na ubora ule ule kwa sababu watu wengi wamezoea kuwa bidhaa ikiuzwa kwa bei ya chini basi haina ubora au imepitwa na wakati. Akitoa maoni juu ya kauli hiyo hapo juu, Bi. Asha Mohamed ambaye ni mfanyabiashara alisema kuwa, "Nakumbuka mwaka jana shoga yangu alinunua simu ya kisasa kwa bei chee kabisa lakini sikuamini jinsi ilivyokuwa na ubora wa hali ya juu. Safari hii nimejionea mwenyewe ni kweli Vodacom wameamua sasa kila mtu lazima amiliki smartphone.
 Kundi la TMK Dancers wakiburudisha wateja waliojitokeza katika gulio la Vodacom Expo lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii. Gulio hilo liliandaliwa naVodacom Tanzania kwa kushirikia na wadau wa kampuni za mawasiliano liliwapatia wateja wake fursa ya kununua  bidhaa za mawasiliano kwa punguzo la bei nafuu zaidi kwa siku mbili mfululizo za tarehe 28 na 29 za mwezi wa Juni.
 Kundi la TMK Dancers wakiburudisha wateja waliojitokeza katika gulio la Vodacom Expo lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii. Gulio hilo liliandaliwa naVodacom Tanzania kwa kushirikia na wadau wa kampuni za mawasiliano liliwapatia wateja wake fursa ya kununua  bidhaa za mawasiliano kwa punguzo la bei nafuu zaidi kwa siku mbili mfululizo za tarehe 28 na 29 za mwezi wa Juni.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mabibo, Ester Michael (katikati) akifurahia zawadi ya simu ya smartphone ya Vodafone aliyojishindia mara baada ya kununua bidhaa kwenye gulio Vodacom Expo. Gulio hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki hii kwa siku mbili mfululizo za tarehe ya 28 na 29 ya mwezi Juni katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.