UBELGIJI, moja ya timu cheche zinazoundwa na wachezaji vijana kwenye Kombe la Dunia, wamefanikiwa kutinga hatua ya 16 ya michuano hiyo baada ya kuifunga Urusi 1-0.
Kwa kushinda mchezo huo Ubelgiji inajisukanyia pointi 6 na kujihakikishia nafasi ya kwanza kwenye kundi H hata kama itapoteza mchezo wake wa mwisho.
Bao pekee la Ubelgiji lilifungwa dakika ya 88 na kinda Divock Origi aliyeingia kuchukua nafasi ya Lukaku aliyechemsha vibaya kwenye mchezo huo.
Beki wa kati wa Ubelgiji Thomas Vermaelen ambaye anahusishwa na uhamisho wa kwenda Manchester United akadhihirisha kuwa bado tatizo la kuwa majeruhi halichezi mbali na yeye baada ya kuumia na kutolewa dakika ya 30.
Nafasi wa Vermaelen anayeichezea Arsenal ilichukuliwa na beki wa Tottenham Vertonghen.
Belgium 4-3-2-1: Courtois 7.5; Alderwiereld 6.5, Van Buyten 6, Kompany 6.5, Vermaelen 5 (Vertonghen 30mins, 5.5); Witsel 6, Fellaini 5, Mertens 8 (Mirallas 75mins, 6.5); De Bruyne 6.5, Hazard 6; Lukaku 3.5 (Origi 55mins, 7).
Russia 4-1-1-3-1: Akinfeev 7.5; Kozlov 5.5 (Eshchenko 65mins, 6), Berezutskiy 6.5, Ignashevich 5.5, Kombarov 6; Glushakov 7; Fayzulin 6.5; Samedov 5 (Kerzhak 90mins), Kanunnikov 6, Shatov 5 (Dzagoev 83mins); Kokorin 6.