MAREHEMU REDEMPTA
KATONDAABELA (MAMA RWEKAZA)
Familia ya Prosper Mutafurwa wa Mtaa wa Mwale, Tandika Maguruwe, Dar es salaam. Inasikitika kutangaza kifo cha Mke wake mpendwa Redempta KatondaAbela ai Mama Rwekaza (Pichani) kilichotokea alfajiri ya Jumapili tarehe 01/06/2014 akiwa usingizini.
Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki wote popote walipo.
Mipango ya mazishi inafanyikia Nyumbani kwa Mume wa marehemu Tandika Dar es salaam.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa siku ya Jumatano tarehe 04/06/2014 kwenda Katoke, Buyango, Kiziba, Bukoba na mazishi yatafanyika Siku ya Ijumaa tarehe 06/06/2014 huko huko Katoke,Buyango, kiziba, Bukoba.
Glob ya Jamii inatoa pole kwa
familia nzima, ndugu, jamaa na marafiki wote
BWANA AMETOA NA BWANA
AMETWAAJINA LAKE NA LIHIMIDIWE
AMEN