WAWAKILISHI wa bara la Afrika katika kipute cha kombe la dunia, Ivory Coast wameonyesha kuwa ni washindani wa kweli ndani ya michuano hii inayoendelea nchini Brazil kwa kutandaza soka la hali ya juu dhidi ya Colombia.
Katika mchezo huo, licha ya Ivory Coast kufungwa 2-1 'kwa bahati mbaya' walikuwa tishio kwa Colombia na kuonyesha kuwa bado wana nafasi ya kusonga mbele kama watashinda mchezo wao wa mwisho kati yake na Ugiriki.
Ivory Coast ilicheza soka tamu huku ikiishambulia Colombia kwa karibu muda wote wa mchezo lakini walikuwa na upungufu wa mbinu za kukwamisha mipira wavuni.
Colombia walicheza zaidi kwa kutibua 'muvu' za mwisho za Ivory Coast pamoja na kutengeneza mashambulizi ya kushtukiza jambo ambalo liliwanufaisha.
Kama anajichulia vile Geffroy Die akilia wakati wimbo wa taifa ukipigwa
Bao la kwanza la Colombia lilikuja dakika ya 64 kupitia kwa Rodriguez huku bao lao la pili likifungwa na Quintero kunako dakika ya 70.
Hata hivyo ni bao la kufutia machozi la Ivory Coast lililofungwa na Gervinho ndio lililokuwa tamu zaidi pale alipoichambua safu ya ulinzi ya Colombia na kufunga kwa mkwaju mkali dakika ya 73.
Bao la kwanza
Rodriguez baada ya kuifungia Colombia bao la kwanza
Colombia wakishangilia bao
Gervinho akiifungia Ivory Coast
Baada ya hapo Ivory Coast iliendelea kulisakama lango la Colombia kwa kusukuma mashambulizi mengi lakini bado walishindwa kujiokoa na kipigo.
Majina makubwa kama Yaya Toure, Didier Drogba na Wilfried Bony yalishindwa kuonyesha ubora wao na laity kama wachezaji hao wangekuwa kwenye kiwango chao cha kawaida, basi shughuli ingekuwa pevu kwa Colombia.
Colombia: Ospina 6, Armero 7 (Arias 72), Yepes 7, Zapata 6, Zuniga 6, Sanchez 6 Moreno 6, Aguilar 6 (Mejia 78), Ibarbo 6 (Quintero 53 7), Rodriguez 7, Cuadrado 8, Gutierrez 6.
Ivory Coast: Barry 6, Boka 6, Bamba 6, Zokora 5, Aurier 7, Die 6 (Bolly 73), Tiote 6, Gervinho 6, Yaya Toure 6, Gradel 6 (Kalou 67 7), Bony 5 (Drogba 60 5).