Sunday, June 08, 2014

PICHA KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA:MKUU WA WILAYA YA NKASI AZINDUA HUDUMA YA OPTION B PLUS MKOANI RUKWA (TIBA YA KUZUIA MAAMBUKIZI YA VVU KUTOKA KWA MAMA MJAMZITO KWENDA KWA MTOTO MCHANGA)




PICHA KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA:MKUU WA WILAYA YA NKASI AZINDUA HUDUMA YA OPTION B PLUS MKOANI RUKWA (TIBA YA KUZUIA MAAMBUKIZI YA VVU KUTOKA KWA MAMA MJAMZITO KWENDA KWA MTOTO MCHANGA)
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi huduma ya Option B Plus Mkoani Rukwa jana tarehe 07 Juni, 2014 katika Kijiji cha Tamasenga Wilayani Sumbawanga. Huduma hiyo ina lengo la kutoa tiba ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto mchanga. Kaulimbiu ya huduma hiyo ikiwa "Amka Sasa Tokomeza VVU kwa Watoto, Kama mjamzito Pima VVU kwa maisha Bora, Tiba inapatikana"
Mkuu wa Wilaya Nkasi Iddi Hassan Kimanta (kulia) akipokea taarifa ya utaratibu maalum na tiba ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto mchanga kutoka kwa wataalamu wa tiba alipotembelea banda la Hospitali Kuu ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa muda mfupi kabla ya uzunduzi wa huduma hiyo katika viwanja vya Tamasenga Wilayani Sumbawanga. Katika salam zake Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wahudumu wa afya kuzingatia viapo vyao kwa kutunza siri za wagonjwa hususani walipomwa na kukutwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akisoma risala kwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ya uzinduzi wa huduma ya Option B Plus. Katika risala yake amesema maambukizi ya virusi vya Ukimwi Mkoani Rukwa yameongezeka ambapo sasa yapo kwa kiwango cha asilimia 6.2. Alisema mpaka sasa jumla ya watumishi 225 sawa na asilimia 75% wameshapatiwa mafunzo ya utoaji wa huduma hiyo ambapo matarajio ni kufikia watumishi 302. Alieleza kuwa mpaka sasa jumla ya vituo 116 vinatoa huduma hiyo sawa na asilimia 83% lengo likiwa kufikia vituo 139 hadi kufikia mwezi Septemba 2014.
Hafla hiyo ya uzinduzi ilipambwa na maandamano ya awali yaliyokuwa yakitoa ujumbe wa mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto mchanga. 
Meza kuu ikipokea maandamano hayo kwa kupiga makofi. Wakwanza kushoto ni Naibu Meya Manispaa ya Sumbawanga,  Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Erasmus Rugarabamu, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta na Mganga Mkuu Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha kushoto akiteta jambo na Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Rukwa Dkt. Hansi Ulaya muda mfupi kabla ya uzinduzi wa huduma hiyo.
Baadhi ya wadau wa huduma ya afya waliohidhuria katika hafla hiyo.
Picha na -Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa