Tuesday, June 24, 2014

MAADHIMISHO YA KILELE CHA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA KUFANYIKA KITAIFA MKOANI MBEYA.




MAADHIMISHO YA KILELE CHA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA KUFANYIKA KITAIFA MKOANI MBEYA.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya kilele cha kupambana madawa ya kulevya yatakayofanyika mkoani Mbeya

Baadhi ya wandaaji wa maadhimisho hayo wakimsikiliza mkuu wa mkoa Mbeya


Waandishi wa mkoa wa Mbeya wakimsikiliza mkuu wa mkoa Mbeya








MAADHIMISHO ya kilele cha kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya yanatarajiwa kufanyika kitaifa mkoani Mbeya ambapo Makamu wa Raisi, Dk. Mohamed Gharib Bilal atakuwa mgeni rasmi.

Maadhimisho hayo yatafanyika katika viwanya vya Shule ya Msingi RuandaNzovwe Ilomba jijini Mbeya Juni 26, Mwaka huu.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuiasa jamii na kuikumbusha kuhusu athari za matumizi ya madawa ya kulevya kwa kukataa kuuza wala kuingiza nchini.

Amesema Mkoa wa Mbeya umepata nafasi ya kuandaa sherehe hizo kutokana na kuwa Mkoa unaopakana na nchi jirani hivyo kuwepo kwa mwingiliano mkubwa na upishaji wa madawa ya kulevya kutoka nchi za Nje ambazo zinapakana na Mkoa wa Mbeya.

Kandoro amesema kauli mbiu ya Mwaka huu ni "Uteja wa dawa za kulevya unazuilika na kutibika chukua hatua".
Aliongeza kuwa maadhimisho hayo yalianza Juni 24, Mwaka huu na kufikia kilele Juni 26, Mwaka huu ambapo shughuli mbali mbali zimaenza kufanyika zikiwemo za upimaji, utoaji elimu na kutoa matibabu kwa waathirika wa madawa ya kulevya.

Aidha amezitaja baadhi ya taasisi zinazoendelea na zoezi hilo kuwa ni pamoja na Mkemia mkuu wa Serikali, Mamlaka ya chakula na dawa(TFDA),Hospitali ya Mkoa wa Mbeya,Hospitali ya Rufaa ya Mbeya,Mashirika binafsi na Jeshi la Polisi.

Mwisho.

Na Mbeya yetu