Sunday, June 22, 2014

Kampeni ya Uchangiaji damu iliyoendeshwa na Diwani wa Kipawa,Mh. Bonna Kaluwa yafikia tamati leo



Kampeni ya Uchangiaji damu iliyoendeshwa na Diwani wa Kipawa,Mh. Bonna Kaluwa yafikia tamati leo
Meya wa Ilala, Jerry Silaa akifungua rasmi tamasha la kuchangia damu katika viwanja vya Stakishari, Majumbasita, Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo ya siku 10 iliratibiwa na Diwani wa Kipawa Bonnah Kaluwa (CCM).
Meya Silaa akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Damu Salama kabla ya kuchangia damu ili kuwaokoa wagonjwa wakiwemo wakina mama wajawazito katika viwanja vya Sitakishari Majumbasita, Dar es Salaam.
Meya Silaa na Diwani Bonnah wakiendelea kusikiliza maelezo kutoka kwa maofisa wa damu salama kabla ya kuchangia damu ili kuwaokoa wagonjwa wanaoteseka mahospitali kwa kukosa damu.
Meya wa Ilala, Jerry Silaa akiugulia maumivu ya sindano wakati akitoa damu ili kuwaokoa wagonjwa wanaohitaji damu katika hospitali mbalimbali wakiwemo wajawazito bila kuwasahau madereva na abiria wa bodaboda wanaoandamwa na ajali.
Diwani wa Kipawa, Bonnah Kaluwa naye akidhihirisha azma yake ya kuchangia damu kwa vitendo katika kilele cha kampeni yake ya kuchangia damu jana katika viwanja vya Sitakishari, Majumbasita ambapo mamia ya wakazi wa Dar es Salaam walijitokeza.
Mwakilishi wa Chuo cha Diplomasia, Kennedy Ndosi (katikati) aliyewahamasisha wanafunzi wa Chuo hicho waliofika kuchangia damu akiwasikiliza Meya Silaa na Diwani Bonnah wakati wa tamasha hilo.