Mabingwa watetezi Bilele FC wameanza kwa kufungua Michuano hii ya Kagasheki Cup vibaya baada ya Kutandikwa bao 3-1 na Timu ya Rwamishenye Fc leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini. Bilele FC ndio walioanza kuifunga timu ya Rwamishenye katika dakika ya 5 kipindi cha kwanza, Bao likifungwa na Miraji Ramadhan.
Timu ya Rwamishenye waliongeza bidii ili wasawazishe bao na katika dakika ya 20 kipindi cha kwanza walisawazisha bao kupitia kwa mchezaji wake Khalid Seleman na kuongeza tena bao jingine katika dakika ya 42 kupitia kwa Yahaya Sadiq aliyekuwa amevaa jezi namba 7 mgongoni na kufanya 2-1 dhidi ya timu ya Bilele Fc yenye makazi yake Bukoba Mjini wakifaamika zaidi kwa jina la KM.0, hadi mapumziko Rwamishenye ndio walikuwa mbele ya bao 2-1. Kipindi cha Pili dakika ya 56 walioshona tena bao jingine la mwisho kupitia kwa mchezaji wake matata Edwin Edo na kufanya kipute kumalizika kwa bao 3-1.
Kesho Mtanange unaendelea na utazikutanisha timu za Bakoba na Kashai, Mtanange utakao pigwa saa 10:00 jioni. Jumatatu kutakuwepo na mitanange 2 wa saa 8 na saa 10 jioni.Wachezaji wa Rwamishenye Fc wakishangilia moja ya bao laoWachezaji wa timu ya Bilele Fc wakishangilia bao lao la dakika ya 5 lilifungwa na Miraji RamadhanKikosi Cha Timu ya Rwamishenye kilichoanzaKikosi cha Timu ya Bilele FCTimu zikisalimianaWaamuzi na Timu Kapteni timu zote mbili wakilianzisha Waamuzi wa Mtanange huuKikosi cha Timu ya Rwamishenye uwanjani wakiomba kabla ya kipute kuanza muda mfupiMgeni Rasmi akisalimia timu ya RwamishenyeMgeni Rasmi akisalimia timu ya Bilele Fc ambao ndio Mabingwa watetezi wa Kombe hiliMgeni Rasmi akiteta jambo na Wachezaji Pande zote mbiliMashabiki wakishangilia timu yaokipute kikiendelea..kaitabaWachezaji wa Timu ya Bilele walivalia jezi zinazofanana na Mbeya CityPatashika za hapa na pale zikiendelea, kila mchezaji akitaka aupate mpiraKila Mchezaji alikuwa na mwenzake wakubanana nae.Hapa ukatizi ndugu yangu!Wachezaji wa Timu ya Rwamishenye wakicheza muziki baada ya kusawazishaMashabiki ndio usiseme...walifujaa uwanjani KaitabaMashabiki
Waamuzi wakina Dada nao walikuwepo wakitazama wenzao wakiendesha mpira
Mchezaji wa Rwamishenye akishangilia bao lake la pili lililofungwa na Yahaya
Wachezaji wa Rwamishenye wakishangilia bao lao baada ya kuwanyuka Bilele Fc