Wakazi wa Zanzibar wako katika hali ya wasiwasi baada ya kushuhudia tukio lengine la kulipuka bomu kwa viongozi wa dini huku safari hii likiua kijana mmoja na kujeruhi saba.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa upelelzi na makosa ya jinai zanzibar Sacp Yussf Ilembo, bomu hilo lilitupwa na mtu au watu wasijulikana ambao walikuwemo ndani ya gari lilkuwa halina namba za usajili ..Ilembo amesema kuwa bomu hilo lilitupwa kwa kikundi cha wananchi waliokuwa pamoja na viongozi wa dini ambao walikuwa wametoka msikitini na wamesimama nje ya gari.
Kijana mmoja Mohamed khatibu Mkombalaguha ambaye ni mkaazi wa pongwe Tanga aliyekuja Zanzibar kwa ajili ya hitima alifariki hapo hapo na wengine saba akiwemo Sheik Kassim Mafuta wamejeruhiwa...
Nao baadhi ya majeruhi Ahmed Haidar na mwanawe khalid Ahmed wakiongea wakiwa wamelazwa hosptali ya Alrahma wamesema hawajui wala hawakumuona mtu ailyerusha bomu hilo, wao wameshtukia mlipuko mkubwa .
Mkurugenzi huyo wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Zanzibar amesema kuwa jeshi la Polisi limeanza kuwasaka waliohusika na mlipuko wa bomu hilo.
source: TBC