Innocent Melleck akikaribishwa na chipukizi katika uwanja wa Ghala -Himo wilaya ya Moshi vijijini kwa ajili ya kusimikwa kuwa naibu kamanda wa UVCCM katika wilaya hiyo.
Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini Dk Cyril Chami (katikati) Innocent Melleck ,Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Moshi vijijini Moris Makoi na viongozi wengine wa CCM wakipunga mkono kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa shughuli ya kumsimika naibu kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi vijijini.
Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini na kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi vijijini Dk Cyril Chami akimvisha vazi maalumu Innocent Melleckak wakati akisimikwa kuwa Naibu kamanda wa UVCCM wa wilaya hiyo.
Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini na kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi vijijini Dk Cyril Chami akimkabidhi Innocent Melleckak ngao na mkuki kuashiria kukabidhiwa majukumu ya kuwa Naibu kamanda wa UVCCM wa wilaya hiyo