Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) utaendesha mafunzo ya siku tatu -Jumatatu 23 -Jumatano 25 Juni 2014, katika ukumbi wa Mabati Jeshi la Kujenga Taifa Mgulani, Temeke, jijini Dar es salaam.
Lengo la mafunzo haya kwa mwaka huu ni kuwaelimisha na kuwawezesha wanawake wajasiliamali jinsi ya kupata mitaji, masoko na kufanya biashara endelevu.
Mada kuu zitahusu: Uwekezaji na Ukuazaji mtaji, Mtaji sio Lazima Uwe Fedha; Utunzaji wa Kumbukumbu za Biashara yako, Kuwaunganisha Wazalishaji na Masoko; Mnyororo wa Bidhaa; Mbinu za kushiriki Maonyesho ya Biashara, Usindikaji na Mazao, Usajili na Matumizi ya "Bar Code" na Elimu na uhamasishajiwa wa maradhi sugu na hatari kwa wanawake yanayorudisha Maendeleo yao – Saratani ya Matiti na Shingo ya Kizazi, Fistula, UKIMWI, Dengue/Malaria na Homa ya Ini.
Watoa Mada ni pamoja na Wajasiriamali maarufu - IPP, Soko la Hisa la Dar-es-salaam- DSE, Wakufunzi kutoka TRA, TanTrade Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam, Madaktari Kutoka CCBRT, Ocean Road, Ilala na Temeke .
Wanawake wote mnakaribishwa kuhudhuria Mafunzo haya yenye lengo la kuwakomboa kiuchumi, Kiafya na kuwakutanisha kubadilishana ujuzi, Uzoefu na biashara.
Hakuna malipo kwa kushiriki.
KARIBUNI
Mkurugenzi Mtendaji,
Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF).
0715 263284
DAR ES SALAAM