Wauguzi wa
Zanzibar wakila kiapo cha Utii katika maadhisho ya siku ya wauguzi Duniani
inayoadhimishwa kila ifikapo tarehe 12 Mei. Maadhimisho hayo yalifanyika
Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongochekundu
Wauguzi wa
Zanzibar wakiimba nyimbo ya siku ya wauguzi Duniani katika maadhimisho
yaliyofanyika Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongochekundu.
Muuguzi Mkuu
Kiongozi wa Zanzibar Bi. Wanu Bakari Khamis akisoma risala ya siku ya wauguzi
Duniani katika maadhimisho yaliyofanyika
Kidongochekundu.
Katibu Mkuu
Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jidawi akimkabidhi zawadi Muuguzi Ramla Kombo wa
Kituo cha Afya Unguja Ukuu kwa kuwa miongoni mwa wauguzi waliofanya vizuri
zaidi mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani yaliyofanyika
Kidongochekundu.
Muuguzi Rajab
Khamis Rajab akipokea zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya ya Zanzibar
kwa kuwa miongoni mwa wauguzi waliotekeleza wajibu wao kwa ufanisi zaidi mwaka
huu.
Wauguzi wa Zanzibar
wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk. Muhammed Jidawi (hayupo
pichani) katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani yaliyfanyika Hospitali ya
wagonjwa wa akili Kidongochekundu. Picha na Makame
Mshenga-Maelezo Zanzibar.