Monday, May 19, 2014

WAHITIMU WA UALIMU WAASWA KUTOKUKIMBILIA KUKOPA

 
 
 


 
  Mgeni rasmi  Meneja Sheria wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma  (PSPF)Taifa,Abrahamu Siyovelwa akizungumza na wahitimu katika mahafali ya chuo cha Mutco yaliyofanyika mwishoni mwa wiki. (picha zote na Denis Mlowe)
Mkuu wa chuo cha Mutco Leuterius Mheni  akisoma taarifa ya chuo mbele ya wahitimu na wageni waalikwa katika mahafali ya kuhitimu astashahada ya ualimu chuoni hapo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika chuo hicho.
Baadhi ya wahitimu wa ualimu wakiwa katika mahafali yao chuoni hapo.
Baadhi ya wahitimu wa ualimu wakiimba wimbo wa kuwaaga wenzao katika mahafali yao chuoni hapo
Na Denis Mlowe,Mufindi

WAHITIMU mafunzo ya Ualimu katika chuo cha Ualimu Mufindi (MUTCO) kilichoko wilayani Mufindi mkoani Iringa wametakiwa kutokukurupuka kukopa katika taasisi mbalimbali za mikopo zinazowafata mara baada ya kupata ajira kwa kuwa zinamalengo ya kuwafanya kuwa maskini na kuishi kwa kukopa na kulipa.
 
Kauli hiyo imetolewa na Meneja Sheria wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma  (PSPF) Taifa,Abrahamu Siyovelwa , aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya tatu katika chuo yaliyofanyika mwisho mwa wiki katika ukumbi wa MUTCO, alisema badala yake wafanye chaguo sahihi wakati wa kukopa na kuangalia na kupitia mikataba kabla ya kujiunga na kuchukua mikopa katika taasisi hizo.
 
Siyovelwa alisema kuwa ni vema watumishi wanaoingia katika ajira mpya kutokukurupuka pindi wanapotaka kukopa katika taasisi mbalimbali za kifedha kwa kuwa baadhi ya tasisi hizo zimejawa na ujanja ujanja katika mikataba yao.
 
"Naowamba sana kuwa makini sana katika kukopa hivyo  ni wakati wa watumishi wapya hususani walimu kufanya chaguo sahihi katika kukopa mtaishi maisha ya kukopa na kulipa hadi mwisho wa kuustaafu kazi na kutolea mfano ukitaka kujua unakokwenda angalia umbali wa ulikotoka hivyo kuwenu makini sana na baadhi ya taasisi " alisema Siyovelwa
 
Aliwataka wahitimu hao kutumia changamoto zilizoko katika mazingira watayopangiwa kuzitumia  kama fursa katika kujiletea maendeleo hasa kwa walimu watakaopangiwa sehemu ambazo huduma za  jamii ni chache na kuzitumia kuwekeza na kuacha kukimbia changamoto hizo

Aidha aliwaasa wahitimu hao kujiunga na PSPF kwa kuwa kuna baadhi ya mafao mbalimbali yanayotolewa na mfuko  huo yanalenga kuwawezesha watumishi kukabilina na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utumishi wao kabla na baada ya kustaafu
 
Siyovelwa alisema PSPF ina mpango imeweka  mahususi wa kuhakikisha unaboresha maisha wa wanachama wake wakiwemo walimu hivyo kuwataka kuwekeza kwa faida ya maisha yao.
 
Katika mahafali hayo mfuko huo wa PSPF umechangia mabati 100 yenye thamani ya sh. Milioni 1.8 kwa chuo hicho kwa lengo la kukamilisha baadhi ya majengo ya chuo hicho ambayo hayajakamilika.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Leuterius Mheni  amesema kuwa chuo hicho kilianza rasmi mwa 2010 na jumla ya wahitimu 64 kati ya wahitimu 76 wa cheti cha astashahada.

Alisema chuo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo huduma ya maji na vifaa vya kufundishia, ambapo uongozi wa chuo umekuwa likifanyia jitihada za kuzitatua mara pesa inapopatikana.

Katika risala yao wahitimu wamesema kuwa ualimu sio jalala la watu walioshindwa hivyo wameipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kutoa mtaala mpya utakaosaidia ubora wa elimu nchini kwa kuchukua walimu wenye sifa na waliosomea mafunzo ya ualimu.