Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa Akitoa hotuba ya ufunguzi wakati wa kikao cha kupitia Mpango Mkakati wa Takwimu za Kilimo kilichojumuisha maafisa waandamizi kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar pamoja na Wadau wa Maendeleo nchini. Kikao hicho kimefanyika juzi katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. |
Mratibu wa Mpango Kabambe wa Kitaifa wa Kuimarisha na Kuboresha Takwimu Nchini akiwasilisha mada juu ya utekelezaji wa mpango huo wakati wa kikao cha kupitia Mpango Mkakati wa Takwimu za Kilimo kilichojumuisha maafisa waandamizi kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar pamoja na Wadau wa Maendeleo nchini. Kikao hicho kimefanyika juzi katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. |
Meneja wa Takwimu za Kilimo Bw. Titus Mwisomba akiwasilisha Mpango Mkakati wa Takwimu za Kilimo kwa maafisa waandamizi kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar pamoja na Wadau wa Maendeleo nchini wakati wa kikao cha kupitia mpango huo kilichofanyika juzi katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. |
Baadhi ya maafisa waandamizi kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar pamoja na Wadau wa Maendeleo nchini wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kupitia Mpango Mkakati wa Takwimu za Kilimo kilichofanyika leo katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.Picha zote na Veronica Kazimoto |