Monday, May 26, 2014

Mshauri wa Masuala ya Ulinzi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro afanya ziara ya kikazi katika visiwa vya Comoro




Mshauri wa Masuala ya Ulinzi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro afanya ziara ya kikazi katika visiwa vya Comoro
Mshauri wa Masuala ya Ulinzi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro mwenye makazi yake Mjini Maputo, Msumbiji, Kanali Mahamud Lwimbo, alifanya ziara ya kikazi katika visiwa vya Comoro ambapo alikutana na Viongozi Wandamizi wa Visiwa hivyo wakiwemo Mhe. Ahmada Mmadi Bolero, Waziri anayehusika na Masuala ya Ulinzi na Kanali Youssouf Idjihadi Mkuu wa Jeshi la Comoro. Alipokutana na Viongozi hawa wa Comoro, Kanali Lwimbo alipata fursa ya kuzungumzia kwa kina umuhimu na namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya Ulinzi baina ya Tanzania na Comoro.
Kanali Lwimbo (kushoto), Mshauri wa Masuala ya Ulinzi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro akimkabidhi zawadi Mhe. Bolero, Waziri wa Ulinzi wa Muungano wa Visiwa vya Comoro.
Kanali Lwimbo akiwa na Mkuu wa Majeshi wa Comoro.
Kanali Lwimbo akiwa pamoja na Waziri wa Ulinzi na Mkuu wa Majeshi wa Comoro.