Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na watanzania waishio nchini Japan, wakati alipokutana nao kwa mazungumzo yaliyofanyika kwenye Hoteli ya The New Otani, wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi nchini humo, jana Mei 21, 2014. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Japan (Tanzanite Society) David Semiono, akisoma risala ya Jumuiya yao wakati wa hafla ya chakula cha jioni na Makamu wa Rais Dkt. Bilal, iliyofanyika kwenye Hoteli ya The New Otan, jijini Tokyo Japan, jana usiku Mei 21, 2014.
Baadhi ya Watanzania waishio nchini Japan, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa wakiwahutubia katika hafla ya chakula cha jioni, iliyofanyika kwenye Hoteli ya The New Otan, jijini Tokyo Japan, jana Mei 21, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na mwanamuziki Mtanzania wa bendi ya The Tanzanite, Abuu Omar, wakati alipokuwa akiagana na baadhi ya Watanzania waishio Japan, waliohudhuria hafla hiyo ya chakula cha jioni. Kulia ni Mke wa Makamu, Mama Asha Bilal.