Tuesday, May 27, 2014

Know your career exhibition June 28, 2014 at National Museum and House of Culture, Dar es salaam




Know your career exhibition June 28, 2014 at National Museum and House of Culture, Dar es salaam
Utafiti umeonesha ya kuwa moja ya chanzo cha matatizo ya ajira ni ukosefu wa utambuzi au uelewa wa kazi ni nini. Wengi tumekuwa tukisoma kwa bidii ili tufaulu tuje tuajiriwe lakini wengi wetu hatujui ni kazi gani haswa tunazipendelea, zaidi ya hayo hatutambui ni kazi gani zinaendana na tabia zetu. 
Inakubalika ya kuwa watu wanaofanya kazi zinazoendana na personality na ujuzi wao huwa wanazalisha zaidi ukilinganisha na wale wanaofanya kazi ili tu mkono uende kinywani. 
Mbali na hayo, ukifanya kazi unayoipenda na inayokufa itakuongeze furaha kazini ivo kukupa maisha bora na afya bora. Ieleweke ya kuwa swala zima la kuchagua aina la kazi linaanzia ngazi za chini kabisa yaani kidato cha nne.
Tamasha hili pia linalenga kuwahamasiha vijana kuhusu ajira mbali mbali km photography, hair stylists, designers, graphic designers, chefs n.k. Soko la ajira linapanuka, ukuwaji wa sayansi na teknolojia umefungua milango kwa shughuli mbali mbali. 
Tunaalika makampuni yote yenye kujihusisha na kazi za mikono, wajasiriamali wote, cooperate companies na vyuo vyote vyenye kutoa mafunzo ya kazi za mikono au short courses kushiriki katika tamasha hili la kwanza na la kipekee litakalojenga Tanzania bora zaidi.

KWA MAELEZO ZAIDI YA TAMASHA NA USHIRIKI PIGA SIMU NAMBA0789250580 au BARUA PEPE info@inspirit.co.tz