Saturday, May 24, 2014

KINANA:CHAMA KINAWAJIBU WA KUHAKIKISHA KINATIMIZA AHADI ZA 2010



KINANA:CHAMA KINAWAJIBU WA KUHAKIKISHA KINATIMIZA AHADI ZA 2010


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Iramba Magharibi wakati wa mapokezi katika kijiji cha Kiselya. Katibu Mkuu na msafara wake wameanza ziara katika wilaya ya Iramba kwa lengo la kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 pamoja na kukagua uhai wa chama. 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kubeba mawe ya ujenzi wa kituo cha afya cha Kiselya, wilaya ya Iramba kwa kushirikiana na viongozi wengine pamoja a wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Kiselya, wilayani Iramba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipitia daftari la wanachama nyumbani kwa Balozi wa shina Julius Said wa kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimimina zage wakati wa kushiriki ujenzi wa kituo cha afya Shelui,wengine wanaosaidiana nae ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Mwigulu Nchemba na Mbunge wa Viti Maalum Martha Mlata.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba (kulia) na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Shelui mkoani Singida.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Shelui kwenye mkutano wa hadhara na kuwaambia CCM ina kila sababu ya kuzunguka na kukagua miradi ya serikali kwani ndio yenye ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010 ndio iliahidi hivyo lazima ikague kuhakikisha utekelezaji wake.
 Kila mtu ana haki ya kusikiliza mkutano wa CCM bila kujali itikadi za chama ulichotoka,kijna akiwa na sare za Chadema akifuatilia kwa makini mkutano wa CCM uliokuwa ukifanyika Shelui.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Naibu Katibu Mkuu CCM (Bara) wakinywa juisi ya parachichi mara tu baada ya kumaliza mkutano wa hadhara Shelui.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Lameck Nchemba akimtambulisha Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwa wananchi wa Misigiri wakati wa kushiriki ujenzi wa ofisi ya Tawi Misigiri.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Iramba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Mwigulu Nchemba wakati wakiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa hadhara Kiomboi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kiomboi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapo na kuwaambia wananchi hao hakuna sababu ya kubadilisha viongozi kama mashati wakati kazi zao za kimaendeleo zinakubalika katika jamii.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kiomboi mkoani Singida na kuwaambia kuwa CCM inaimarika kiasi kila kona zinajengwa ofisi,tofauti na wapinzani ambao wengi ofisi zao zipo mifukoni.
Chumba cha Maabara ya Biolojia cha shule ya sekondari Lulumba iliyopo Kiomboi mkoani Singida,Serikali ya Chama cha Mapinduzi inazidi kuboresha elimu kwa kujenga maabara katika kila sekondari ya kata nchini.