Thursday, May 29, 2014

HAPINESS MAGESE KUTOA MAFUNZO KUHUSIANA UGONJWA WA ‘Endometriosis’




HAPINESS MAGESE KUTOA MAFUNZO KUHUSIANA UGONJWA WA 'Endometriosis'
Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania na aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2001,Hapiness Millen Magese akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro,jijini Dar es Salaam Mey 28,2014 kuhusu kuanzishwa kwa Kampeni ya kuhamasisha wanawake na vijana kupaza sauti zao wanaposumbuliwa na ugonjwa wa 'Endometriosis' baada ya yeye kuathirika na Ugonjwa huo kwa kipindi kirefu.ambapo amesema wanawake wengi na wasichana wamekuwa wakisumbuliwa lakini hawajui kama ni tatizo kubwa linalohitaji utafiti mapema kwa ajili ya kutafuta suluhisho. "Huu ni ugonjwa ambao umenitesa kwa muda mrefu na umeniathiri leo siwezi kuolewa kwasababu sina uwezo wa kubeba mimba, ni mwanaume gani atakubali kukaa na mwanamke asiyezaa, wakati nikiwa mdogo sikujua ni tatizo kubwa, sasa kila siku ninaumwa"alisema Magese. Jumapili ya wiki hii watatoa mafunzo kwenye fukwe za Coco beach ambapo watu wataelimishwa athari na nini kifanyike ikiwa watagundulika kusumbuliwa na tatizo hilo.
Daktari bingwa wa masuala ya wanawake na uzazi 'Endometriosis' wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk. Belinda Balanda,  akielezea seli za mji wa uzazi zinazokuwa nje ya uzazi ambazo hushambulia eneo hilo na kumsababishia mwanamke maumivu makali wakati wa mzunguko wa hedhi.
Wadau kutoka sekta mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.