Thursday, May 15, 2014

BREAKING NEWS!!!: AMINA NGALUMA AFARIKI DUNIA

 
BREAKING NEWS!!!: AMINA NGALUMA AFARIKI DUNIA

MMOJA wa waimbaji nyota wa muziki wa dansi waliowahi kutokea hapa nchini, Amina Ngaluma, amefariki dunia muda mfupi uliopita.

Mwimbaji huyo aliyetamba sana na bendi za Tam Tam na Double M Sound amefia nchini Thailand alipokuwa akiishi kikazi kwa muda mrefu.

Mtu mmoja wa karibu na Amina Ngaluma, Mwanahamisi Omary wa Dar es Salaam

ameimbia Saluti5 kuwa mwimbaji huyo amefariki baada ya kuugua kwa siku kadhaa.

Moja ya nyimbo zilizompatia sifa nyingi Amina Ngaluma ni "Mgumba No 1" aliouimba na bendi ya African Revolution "Tam Tam" chini ya Mwinjuma Muumin.

Ukiingia kwenye ukurasa wake wa Facebook, utakutana salam nyingi za pole na zinazomtakia mapumziko mema milele.

Tutaendelea kukujuza kitakachojiri.