Saturday, May 24, 2014

Basi la UDA lapiga mweleka eneo la Tabata Shule




Basi la UDA lapiga mweleka eneo la Tabata Shule usiku huu
 Moja ya mabasi yanayotoa huduma ya usafirishaji wa abiria ndani ya jiji la Dar es salaam (UDA),lenye nambari za Usajili T 485 CVP na lenye nambari ya idadi 168.usiku huu limepiga mweleka katika eneo la Tabata Shule,mbele ya Hoteli ya Green Light na ubavuni kabisa mwa kituo cha Polisi Tabata.Kamera ya Glogu ya Jamii ilifika eneo hilo na kukuta baadhi ya wahusika waliokuwa wakilitumia basi hilo wakihangaika kutoa baadhi ya mali zao zilizokuwemo ndani ya basi hilo ili waweze kuondoka nazo kwa ajili ya usalama wa mali hizo.Ripota wetu aliposogea na kuwauliza nini chanzo mpaka basi hilo limepiga mweleka huo,hakuna alietaka kujibu swali hilo huku wengine wakijaribu kuipa mgongo kamera yetu.ripota wetu hakuchoka,akajaribu kuwauliza baadhi ya mashuhuda waliokuwepo jirani na eneo la tukio hilo ambao walionekana kulalamika sana huku wengine wakitupia lawama Dereva wa basi hilo kwa kusema "Huu ni uzembe wa Dereva,maana ametaka kusimama gari katika sehemu isiyokuwa na kituo kwa kuchukua abiria mmoja na matokeo yake amesababisha hasara kwa kampuni yake".hivyo ndivyo walivyokuwa wakisika mashuhuda hao.Hadi Tunaondoka eneo la tukio hakukuwa na juhudi zozote za kuliinua basi hilo na wame wahusika waliokuwepo waliondoka.
 Basi hilo likiwa limepiga ubavu.