Saturday, April 20, 2013

'Jeshi lawaua wauguzi' Sudan Kusini



 19 Aprili, 2013 - Saa 11:37 GMT

Wauguzi watano wameuawa Sudan Kusini baada ya wanajeshi kushambulia hospitali moja kulipiza kisasi kwa mauaji ya wanajeshi wengine wanane.

Hii ni kwa mujibu wa mbunge mmoja wa eneo hilo.

Taarifa zinazohusiana

David Mayo alisema kuwa makabiliano yangali yanaendelea na ameitaka serikali kuamuru jeshi kuondoka katika eneo hilo.

Viongozi wa kijamii wamethibitisha hospitali hiyo iliyoko katika jimbo la Eastern Equatoria ilishambuliwa ingawa taarifa kutoka ofisi ya gavana wa jimbo hilo imekanusha habari hizo.

Amesema kuwa jeshi lilikwenda pale kulinda raia.

Ufyatulianaji wa risasi kiholea.

Wanajeshi walipelekwa katika eneo hilo, baada ya walinzi wanane wa gavana wa jimbo hilo kuuawa walipotumwa kuwasaka wezi wa mifugo.

Mwandishi wa BBC wa maswala ya Sudan Kusini Nyambura Wambugu anasema kuwa wakaazi wengi wa eneo hilo lenye milima wamejihami vikali wakiwa na maguruneti ambayo yalianguka mikononi mwao kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miongo miwili.

Bwana Mayo alisema kuwa wanajeshi 13 wanapokea matibabu mjini Torit.

Lakini amelaumu wanajeshi kwa mashambulizi hayo, akisema kuwa waliwafyatulia risasi watu kiholea walipowasili katika eneo la Lorema, kabla ya kushambulia hospitalini hiyo na kisha kuteketeza makaazi ya watu.

Daktari mmoja , mgonjwa mmoja na wauguzi wanne waliuawa.