MARA kwa mara jamii imekuwa ikisikia Wanajeshi wakiwapiga Askari wa Usalama barabarani hasa Jijini Dar es Salaam Trafiki wa Moshi huenda wamechoshwa na unyanyasaji huo kwa walinzi hawa wa amani na wasimamizi wa sheria ambapo huko Mkoani Kilimanjaro, Askari wa kikosi cha usalama barabarani mjini Moshi ambao majina yao hayakufahamika walimpiga askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kituo kikuu cha mabasi hivi karibuni,baada ya kutokea kutoelewana,mwanajeshi huyo alikuwa akimtetea dereva wa Hiace aliyeshikwa na trafiki hao kwa kufanya kosa la kiusalama barabarani.jambo hili halikuwa la kawaida kuonekana machoni mwa watu lakini hivi ndivyo ilivyokuwa.Picha na Nakajumo James wa FK Blog.