Friday, October 12, 2012

Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Saidi Ali Mbarouk akutana na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Diane Conrner


   Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk wamwanzo kulia akimpa zawadi Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Diane Conr ner Baada ya kufanya Mazungumzo kuhusiana na mambo mbalimbali ya Michezo na maendeleo ya Digital hapo Afisini kwake Kikwajuni Zanzibar.
   -Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk wamwanzo kulia akipeana mikono na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Diane Conr ner Baada ya kufanya Mazungumzo kuhusiana na mambo mbalimbali ya Michezo na maendeleo ya Digital hapo Afisini kwake Kikwajuni Zanzibar.
 Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk wamwanzo kulia akifanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Diane Conr ner kuhusiana na mambo mbalimbali ya Michezo na maendeleo ya Digital hapo Afisini kwake Kikwajuni Zanzibar.
  Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo wakimsikiliza Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Diane Conr ner(hayupo pichani)alipokutana na Waziri wa Habari wa Zanzibar hapo Afisini kwake Kikwajuni.Picha na Yussuf Simai, Maelezo
-
Na: YUSSUF SIMAI.MAELEZO ZANZIBAR
 

Wazi wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk amesema kuwa Zanzibar itahakikisha inaingia katika Mfumo wa Digital kabla ya kufikia tarehe iliowekwa ili kwenda sambamba na mabadiliko ya Ulimwengu. Waziri ameyasema hayo hapo Afisini kwake Kikwajuni wakati alipofanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Diane Conrner .

Amesema licha ya Zanzibar kuingia katika Mfumo wa Digital lakini inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa pamoja na Vifaa na mafunzo kwa watendaji wake. Akizungumzia Sekta ya Utalii Waziri Mbarouk alisema kuwa sekta hio inakua kwa kasi kubwa kutokana na Wawekezaji Binafsi ambao huwekeza Zanzibar na kuweza kuitangaza zaidi katika miji na Nchi tafauti.

Aidha amesema kuwa Serikali inafarijika kuona Watalii wengi kutoka Uingereza na nchi nyengine za Ulaya wanafika Zanzibar na kutembelea sehemu mbalimbali za kihistiria na vivutio vyengine vya Utalii vilivyopo nchini. Nae Balozi huyo Diane Conrner ameipongeza Zanzibar kwa juhudi kubwa inazochukua katika kuimarisha sekta ya utalii na kueleza matumaini yake kuwa sekta hiyo itaendelea kuwa muhimili mkubwa wa uchumi.

Akizungumzia sekta ya michezo Balozi Diane ameishauri Serikali ya Mapinduzi ya ZanzĂ­bar kushiriki michezo mbali mbali ikiwemo ya Kimataifa kwa vile michezo inatoa mchango mkubwa katika kuitanga nchi kujulikana duniani kote.

Akitoa mfano wa Michezo ya Olimpiki iliofanyika mjini London, Uingereza, mwaka huu amesema imeweza kuipatia sifa kubwa Nchi yake pamoja na Faida mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Waziri Saidi amemshukuru Balozi huyo kwa Kufika kwake Zanzibar na kuweza kuzungumza na viongozi masuala mbalimbali yenye umuhimu kwa nchi na jamii kwa jumla.