Friday, October 05, 2012

WAZIRI MWAKYEMBE AFUNGUA MKUTANO WA PILI WA LOJISTIKI AFRIKA JIJINI DAR



Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Harrison Mwakyembe akifungua mkutano wa pili wa Lojistiki Afrika,katika Hotel ya Serena.Mkutano huo wa siku mbili umewakutanisha wataalamu mbalimbali kujadili namna bora ya kuboresha Lojistiki katika sekta ya Usafiri.
Mkuu wa chuo Cha Taifa cha usafirishaji(NIT), Mhandisi. Dkt. Zacharia Mganilwa,akitoa salamu zake wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wa pili wa Logistiki Afrika,Mkutano huo unafanyika katika hotel ya Serena,na utafayika kwa siku Mbili huku ukijikita zaidi katika kuboresha Lojistiki katika usafiri wa Reli.
Waziri wa Uchukuzi,Dkt Harrison Mwakyembe akisikiliza kwa makini mada Iliyoeleza umuhimu wa kutumia usafiri wa Reli na namna ambavyo ukitumiwa vizuri unaweza kuongeza pato la Taifa, katika Mkutano wa Pili wa Lojistiki Afrika, mkutano huo wa Siku mbili umewakutanisha wataalamu mbalimbali kutoka Afrika na Nje ya Afrika.Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Bw. John Mndogo(aliyevaa miwani),Na kulia kwa Naibu Katibu Mkuu ni Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji,Mhandisi,Dk. Zacharia Mganilwa.
Baadhi ya wajumbe walioshiriki kwenye mkutano wa Pili wa Lojistiki Afrika unaofanyika kwenye hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.Mkutano huo ulioanza leo unawakutanisha wataalamu mbalimbali wa sekta ya usafirishaji kutoka ndani na nje ya Nchi,wataalamu hao watajadili Mada mbali mbali za kuboressa lojistiki katika Usafirishaji kwa muda wa siku mbili.
Waziri wa Uchukuzi,Dkt Harrison Mwakyembe(wa tano kutoka kushoto),akiwa katika picha ya Pamoja na wataalamu mbalimbali walioshiriki katika Mkutano wa Pili wa Lojistiki Afrika.Mkutano huo wa siku mbili unafanyika katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam na umewakutanisha wataalam mbalimbali wa sekta ya Usafiri kutoka ndani na nje ya nchi.