Monday, October 08, 2012

WAZIRI MKUU MPYA LIBYA ALAZIMIKA KUONDOKA MADARAKANI




 Bunge la nchini Libya limepiga kura ya kutokuwa na imani na kumuondoa madarakani Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo ikiwa muda mchache baada ya Waziri Mkuu Mustafa Abu Shaghur (pichani) kutangaza mawaziri wapya kumi kuendesha nchi hiyo kwa kipindi cha miezi sita ijayo.
Vilevile ilikuwa ni siku chache tu baada ya kulazimika kuliondoa baraza lake la mawaziri kutokana na maandamano ambapo Waziri Mkuu Abu Shaghur alikuwa amechaguliwa na bunge kushika wadhifa huo tarehe 12 Septemba. 2012.
Lakini tangu hapo amekuwa akijaribu kuunda serikali itakayoridhisha makundi yote ya Walibya bila mafanikio.