Wanaoonekana wamevalia fulana za njazo ni baadhi ya wafanya biashara ndogo ndogo za barabarani (Wamachinga) waliopo katika eneo la Mombo mkoani Tanga,fulana hizo ni sare maalum kwa ajili ya kufanyia biashara katika eneo hilo.utaratibu huu ni mzuri kwani hata ikitokea umefanyia ujanja na jamaa hawa inakuwa nirahisi kumpata kwa sababu kila mmoja ana namba yake.
Huyu anauza Mapensheni na ukimuangalia kwenye fulana yake utaona kuna namna isomekayo 079,ambano ni namba yake ya kufanyia biashara katika eneo hilo.
Hawa nao wamepumzika kidogo lakini wako kazini kama kawaida.