Uchaguzi wa jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM, UVCCM mkoani Mara, ulikumbwa na songombingo nguo kuchanika baada ya vijana hao kuzua ugomvi na kupeana kichapo cha nguvu. Kwenye vurugu hizo, licha ya kutwangana ngumi, wadau hao walirushiana viti, mawe na silaha mbalimbali za jadi ndani na nje ya ukumbi wa mkutano jambo ambalo lilisababisha mkutano huo kuvunjika.
Popout
Popout