Thursday, October 18, 2012

TASWIRA ZA JINSI WATUHUMIWA WA VURUGU MAKANISANI MBAGALA WALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI - DAR ES SALAAM

-->

Magari yaliyotumika kuwafikisha washitakiwa waliofanya vurugu, uaribifu na wizi wa mali za makanisa Mbagala, wakiwasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashitaka yanayowakabili.
 Washitakiwa wa kike katika kesi hiyo wakielekezwa kuingia kwenye ukumbi wa mahakama.
 Baadhi ya washitakiwa hao wakipanda basi la polisi kurejea mahabusu baada ya kumalizwa kutajwa kwa kesi yao.

 Hapa wakiwa wamewekwa chini ya ulinzi mkali wa polisi kabla ya kuingia katika moja ya ukumbi mahakamani hapo
 Washitakiwa hao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuingizwa kwenye ukunmbi wa mahakama.
  Mmoja wa askari akiwa katika ulinzi mkali wa kulinda gari lililowapeleka washitakiwa hao mahakamani na kuwarejesha mahabusu.Picha na Dance Francis
 ---
DAR ES SALAAM, Tanzania
WATU 37 wakiwamo wanawake wawili wanaotuhumiwa kuchoma makanisa, kufanya uharibu wa mali na kuiba kwa kutumia nguvu huko Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita, leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya ulinzi mkali.

Washitakiwa hao waliofikishwa mahakamani hapo wakiwa kwenye magari matatu ya polisi aina ya Defender majira ya saa 6:26 mchana chini ya ulinzi mkali wa askari waliokuwa wamevalia mabomu viunoni, kutokana na kufanya matukio hayo kama sehemu ya malipizi yao kutokana na madai ya kunajisiwa kwa mkojo kwa Msahafu kulikofanywa na kijana wa Kikristo.

Baada ya kushushwa, watuhumiwa hao waliamriwa kuchutama kabla ya kuanza kuingizwa kwenye chumba namba moja cha mahakamani hapo, huku kukiwa na tahadhari kubwa ya kiusalama ndani na nje ya mahakama hiyo.

Kwa upande wa mashtaka, watuhumiwa hao wamefunguliwa kesi nne tofauti za jinai kwa mpigo, kesi ya kwanza ni jinai Namba. 240/2012, namba 241/2012, namba 242/2012 na 243/2012.

Watuhumiwa hao walisomewa mashtaka hayo mbele ya Mahakimu Wakazi wawili Sundi Fimbo anayesikiliza kesi tatu huku moja ikisikilizwa na Hakimu Mkazi Bingi Mashabara.

Upande wa Jamhuri kwenye keshi hiyo uliwakilishwa na Wakili Mwandamizi Tumaini Kweka, Lasdlaus Komanya na Joseph Maugo.

Wakili Kweka alidai katika kesi ya jinai namba 243/2012 inayowakabili washitakiwa 17 ambao ni  Maenga Rwenda, Hamad Euli, Shego Sheso, Ramadhani Mgule, Mashaka Iman, Kassim Juma Kigoni, Ibrahim Himu, Hamza Fundi Hamza, Mikidadi  Sadick, Juma Mbegu na Rahimu Boga.

Wengine ni Issa Abdallah, Hamis Kmwaga, Ramadhani Mbulu, Hamed Mohamed, Mohamed Yusuf na Msha Alifa, wanakabiliwa na kosa la kula njama kutenda kosa la  unyang’anyi wa kutumia silaha kinyume na kifungu cha 287A cha sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2012.

Wakili Kweka alidai kuwa Oktoba 12,  mwaka huu huko Mbagala wajatwa waliiba vitu mbalimbali ikiwamo 'Laptop', 'Printer Projector', spika, saa za ukutani na viti vya plastiki vyote vikiwa na thamani ya sh milioni 20 mali ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheli  Usharika wa Mbagala.

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa, kabla ya kuiiba watuhumiwa wamtishia mlinzi Michael Samwel kwa mashoka na nondo kwa lengo la kujipatia vitu hivyo.

Kweka alidai shitaka jingini ni la kuchoma kanisa kinyume na kifungu cha 319(a) cha sheria ya Kanuni ya Adhabu ambapo washitakiwa hao kwania ovu walichoma kanisa hilo mali na kuongeza kuwa shitaka jingine ni la kuharibu mali kama madirisha, meza, mfumo wa umeme, milango, aircondition vyote mali ya kanisa hilo ambavyo vyote vikiwa na thamani ya sh 500,000,000. 

Wakato huo huo, Naye mtoto aliyesababisha vurugu hizo ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Chamazi-Machimbo Mbagala, alifikishwa katika Mahakama ya Watoto mbele ya Hakimu Mkazi  Devota Kisoka  akikabiliwa na kosa moja la kuidhalilisha dini ya Kiislamu  kwa kukikojolea kitabu Qur an Oktoba 10.Chanzo:hakingowiblog