Sunday, October 07, 2012

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI Kuhusu kuuawa kwa Watu wawili Mlowo-Mbozi





WILAYA YA MBOZI - MAUAJI
 
MNAMO TAREHE 04/10/2012 MAJIRA YA SAA 20:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IVUGULA KITONGOJI CHA KIWANI WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA {1} ANDSON S/O MWASHAMBWA, MNYIHA, 51YRS, MKULIMA, MGANGA WA JADI NA {2} BWANASHAMBA S/O MGALA, MNYIHA, 45YRS, MKULIMA WOTE WAKAZI WA MLOWO-RUTUMBI.

WALIUAWA KWA KUPIGWA NA VITU VINAVYODHANIWA KUWA NI MARUNGU/MATOFALI SEHEMU ZA KICHWANI NA USONI NA KUNDI LA WATU WASIOFAHAMIKA KISHA MIILI YAO KUTELEKEZWA SHAMBANI KANDOKANDO YA NJIA YA IVUGULA KWENDA KIJIJI CHA MAHENGE. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI WIVU WA KIMAPENZI AMBAPO MAREHEMU ANDSON S/O MWASHAMBWA AKIWA NA RAFIKI YAKE WALIMKUTA WILLSON S/O WHATSON, MNYIHA, 25YRS, MKAZI WA IVUGULA AKIWA NA MKEWE AITWAYE ANNA D/O KASWISA MAARUFA KWA JINA LA MBUGHI NA KUANZA KUMSHAMBULIA NDIPO KUNDI LA WATU WAKATOKEA NA KUWASAIDIA  KUWASHAMBULIA MAREHEMU ANDSON  NA RAFIKI YAKE BWANASHAMBA .


 MTUHUMIWA WILLSON S/O WHATSON AMEKAMTWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI  NI KINYUME CHA SHERIA NA KWAMBA HATUA KALI ZITAENDELEA KUCHUKULIWA DHIDI YAO. PIA ANATOA RAI KWA JAMII KUJENGA UTAMADUNI WA KUTATUA MIGOGORO YA KIJAMII KWA AMANI LASIVYO INAWEZA KUSABABISHA MAAFA KAMA HAYA.

Signed by;
 [ DIWANI ATHUMANI – ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.