Tuesday, October 02, 2012

SIKU ZA FRANK LAMPARD NA ASHLEY COLE ZINAHESABIKA CHELSEA- ABRAMOVICH.



Na.Mwandishi wetu.
Mmliki wa klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza Roman Abramovich, amesema anatarajia kufanya fagio babu kubwa kwa wachezaji mbalimbali akiwemo Frank Lampard.
Wengine wanaotajwa huenda wakakumbwa na fagio hilo ni pamoja na Ashley Cole na John Terry.
Kwa mujibu wa mtandao wa michezo chini humo, mmiliki huyo ameongeza kuwa fagio hilo litawakumba wachezaji wote wakongwe wenye umri wa zaidi ya miaka 30 waliyopo ndani ya timu yake hiyo.
Ikumbukwe kuwa mchezaji Lampard hadi sasa amefikisha umri wa miaka 34, ambayo ni zaidi ya 30 inayozungumzwa na Abramovich.
Ingawa panga hilo la kutemwa limemwangukia Lampard, bado mchezaji huyo ni lulu kubwa ndani ya Chelsea na yeye binafsi ana imani ndani ya klabu.
Kiungo huyo wa Uingereza anaamini anaweza kubaki endapo ikitokea kama muujiza kutokana na makubwa aliyoifanyia klabu kwa miaka kadhaa ya kuonyesha kiwango murua cha soka.
Kutokana na zengwe hilo ambalo limeshaaza kumuumiza kichwa, ameshauriwa kuanza kuongea na klabu nyingine angalau mwanzoni wa mwezi Januari ajue wapi pa kujificha.
Hata hivyo, kuna tetesi kuwa timu anayokipiga, David Beckham imeshaanza kummendea kwa ajili ya kujiunga nayo kama akihitaji.