Monday, October 08, 2012

NMB yazindua promosheni ya ki-COLLEGE zaidi



Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB Bw. Imani Kajula (kushoto) akitoa ufafanuzi wa promosheni mpya ya Ki-College zaidi kwa viongozi wa vyuo vya elimu ya juu waliohudhuria uzinduzi huo wikiendi hii. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Idara ya wateja binafsi wa NMB Bw. Abdulmajid Nsekela,(pili kushoto) Makamu wa Rais wa chuo cha DUCE, Bi. Kagema Ftain na Makamu wa Rais wa Chuo cha Ardhi Bw. Stephen Mokare.
Viongozi wa Vyuo mbali mbali vya elimu ya juu wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa NMB wakati wa uzinduzi wa kampeni ya NMB Student Account iitwayo Ki COLLEGE zaidi na NMB, hafla hiyo ilifanyika wikiendi hii jijini Dar es Salaam. 
 
NMB ndiyo Benki yenye mtandao mpana wa matawi na ATM nyingi zaidi nchini na imekuwa kinara katika ubunifu Tanzania kwa kuanzisha akaunti zinazokidhi matakwa ya wateja mbalimbali. 

Kwa kutambua jambo hili mwaka 2007, Benki ya NMB ilianzisha akaunti maalumu kwa ajili ya wanafunzi iitwayo NMB Student Account. Akaunti hii ilianzishwa ili kuwawezesha wanafunzi kupata huduma za kibenki kwa urahisi na unafuu zaidi. 

Ki-COLLEGE zaidi na NMB ni promosheni inayowawezesha wanafunzi wenye akaunti ya NMB Student Account kupata nafasi ya kuingia kwenye droo na kujishindia Zawadi mablimbali kama: iPad, Samsung Galaxy, Amana maradufu, flash disk, fulana za NMB, taa inayotumia mionzi ya jua au amana maradufu. Ili uweze kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia zawadi kwenye promosheni ya Ki COLLEGE zaidi na NMB, fungua NMB Student Account, weka amana katika akaunti yako, tumia au jiunge na NMB mobile .

Ikiwa hujatumia akaunti yako kawa muda mrefu tembelea tawi la NMB ili nawe ushiriki katika promosheni hii ya ki-COLLEGE zaidi na NMB. Pamoja na kampeni hii, wanafunzi watakao fungua NMB Student Account wataendelea kufurahia huduma za NMB Student Account kama: 

Kufungua akaunti kwa Sh. 10,000 tu (pamoja na NMB ATM kadi),kujiunga na huduma ya NMB mobile bure kupata huduma ya ujumbe mfupi kila utoapo fedha kwenye ATM ya NMB bure, kuchukua fedha hadi Sh.1,000,000 kwenye NMB ATM kwa siku na kupata huduma kupitia matawi zaidi ya 143 na NMB ATM zaidi ya 450 nchi nzima. Kampeni ya ki-COLLEGE zaidi na NMB iliyoanza rasmi Oktoba 1 itaendelea hadi Desemba 31, 2012.